• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

NYANG’HWALE YAJIDHATITI NA MSIMU MPYA ZAO LA PAMBA 2023/2024

Posted on: May 27th, 2023

Wilaya ya Nyang’hwale imejiandaa vyema na msimu mpya wa zao la pamba 2023/2024 kwa kuhakikisha kunakua na mazingira bora kwa wadau wake wote wanaohusika na zao hilo. Hayo yameelezwa jana Mei 26, 2023 kwenye kikao maalum cha wadau wa zao hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale. Wadau hao ni pamoja na serikali, Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS), wakulima na kampuni za ununuzi wa zao hilo.

Kupitia kikao hiko maalum, Afisa Takukuru Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Stanley Wambura, ameelekeza kufanyiwa kazi kwa changamoto zote zilizojitokeza kwenye misimu iliyopita ya zao hilo, ambazo zinatengeneza mazingira ya watu kujihusisha na vitendo vya rushwa. Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa ugawaji wa pembejeo na uchepushaji wa pembejeo hizo zenye ruzuku ya serikali na hatimae kutowafikia wakulima.

Bw. Wambura ameshauri pia, Watendaji wote wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS), wawekewe dhamana zitakazofidia aina yoyote ya upotevu wa fedha za wakulima. “Kwa kuwa Chama Cha Msingi (AMCOS) ndicho kinachopokea fedha za mkulima kutoka kwa mnunuzi, basi watendaji wake wanatakiwa wadhaminiwe na watu wenye mali zisizohamishika ili kufidia hasara yoyote itakayosababishwa na utendaji kazi wao” Alisema Bw. Wambura

Aidha, Afisa Ushirika Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Jones Rweyunga, aliwasilisha mwongozo Namba 1 wa msimu wa 2023/2024 kuhusu mfumo wa usimamizi na uuzaji wa pamba uliotolewa kwa sheria ya Tasnia ya Pamba namba 2 ya mwaka 2001 na kanuni za Tasnia ya Pamba za mwaka 2011.

“Mwongozo huu unatoa maelekezo ya jumla kwa wadau wote wa Tasnia ya Pamba nchini kuhusu utaratibu wa ununuzi wa pamba kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) katika eneo lililoainishwa. Pia unaweka na kufafanua utaratibu mzima wa mfumo wa ununuzi, usimamizi na uuzaji wa pamba na masharti ya msingi yaliyomo katika Sheria na Kanuni za pamba”. Alieleza Bw. Jones Rweyunga

Nae Mkaguzi wa pamba Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Nicolaus Enos Lutema, alisisitiza “Sitafumbia macho vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uhujumu wa zao hilo, ikiwemo kuweka mawe au mchanga kwenye pamba na kuuza pamba yenye maji”. Aliwaeleza watendaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kampuni za ununuzi, kuhakikisha wanazingatia ubora na usafi wa pamba ya mkulima wakati wote wa ununuzi na usafirishaji.

Mwisho wa mkutano huo, kampuni sita za ununuzi wa pamba zilisaini mikataba na Vyama vyote vya Ushirika vya msingi vya Wilaya ya Nyang’hwale. Kampuni hizo ni ICK COTTON OIL CO. LTD, FRESHO INVESTMENT CO. LTD, AFRISIAN GINNING LTD, KAHAMA COTTON (KCCL) LTD, MAPACHA COTTON CO. LTD na NIDA TEXTILE MILLS LTD 14 (KAHAMA).

Announcements

  • MAPOKEZI YA FEDHA KIASI CHA TSHS 82,298,036.25 YA AWAMU YA KWANZA KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI August 28, 2023
  • TANGAZO LA USAFI WA MAZINGIRA WA KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI August 22, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI 29 ZA KUKUSANYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'HWALE August 17, 2023
  • TANGAZO LA KAZI KWA MAFUNDI UJENZI August 07, 2023
  • View All

Latest News

  • MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI YAFUNGULIWA RASMI GEITA

    September 23, 2023
  • UJENZI WA CHUO CHA VETA KUFUNGUA FURSA KWA VIJANA

    September 20, 2023
  • KAMATI YA SIASA WILAYA YASHAURI WATAALAMU KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    September 18, 2023
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA USAFI DUNIANI YAFANA NYANG’HWALE

    September 16, 2023
  • View All

Video

Ligi daraja la tatu
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved